Maelezo Kuhusu Maonyesho
Muziki wa mdundo unachezwa kichinichini. Tunaweza kuona kuta za rangi ya malai, michoro ya penseli nyeusi na nyekundu kwenye fremu za mbao na okidi inayochanua. Sanamu ndogo ya Brian Chesky, ambayo bado iko kwenye kifurushi chake na sanamu ndogo sana kwenye viweko vya mbao katika sehemu ya mbele. Kwenye fremu ya picha kuna picha ya utotoni ya Brian pamoja na wazazi wake. Sauti ya ubao wa kuongozea.

Mwongozaji
119, tayari.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Skrini imeandikwa, "Nyumba ya Brian. San Francisco, California." Onyesho linabadilika ili kuonyesha ngazi na michoro zaidi ya penseli iliyowekwa kwenye kuta.

Brian anashuka ngazi akiwa na mbwa wake, Labrador mwenye rangi nyeupe na kupiga picha akitumia simu yake. Mlio wa kamera unasikika. Picha inapoonekana vizuri, inaonyesha jiko angavu na lenye nafasi kubwa.

Brian amevaa suruali ya rangi ya mchanga, fulana ya bluu hafifu, raba nyeupe na saa mahiri yenye utepe wa rangi ya chungwa. Kisha mbwa anaketi kwenye kochi na Brian anaendelea kupiga picha huku akishuka ngazi na kuelekea mlangoni.

Skrini imeandikwa, "Brian Chesky. Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Airbnb

Mwongozaji
Hii ni sanaa yako?

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Kuna michoro ya penseli kwenye kuta inayoonyesha nyuso katika mitindo kadhaa

Brian
Brian: Ndiyo, nyingi ni ya shule ya upili.

Mwendeshaji
Unapiga picha za nyumba nzima?

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Brian anatembea-tembea kwenye vyumba mablimbali akipiga picha. Hatimaye, anasimama katika chumba kilicho na ramani ukutani.

Brian
Ndiyo, kwa sababu nitaiweka kwenye Airbnb.

Mwongozaji
Mahali hapa?

Brian
Ndiyo, ninaishi hapa na nitakuwa hapa, ila nitawekachumba hiki kwenye Airbnb.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Katika chumba angavu kilicho na madirisha kwenye kuta mbili, kuna kitanda cha watu wawili kilicho na picha ya jengo la mjini juu ya ubao wa sehemu ya kichwa ya kitanda. Matandiko ni ya rangi ya bluu na nyeupe.

Mwongozaji
Picha hii inamaanisha nini?

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Mwonekano wa karibu wa picha iliyo juu ya ubao wa sehemu ya kichwa ya kitanda unaonyesha nyumba iliyo na madirisha kadhaa mbele, yenye viunzi vya mbao. Brian anakaribia na kunyoosha kidole chake kwenye picha hiyo. Brian anatumia ishara anapozungumza.

Brian
Hapa ndipo yote yalipoanzia. Hapa ni Mtaa wa 19 Rausch, jijini San Francisco. 
Mimi na Joe tulijaza hewa kwenye vitanda 3 tukaviita AirBed na Breakfast na wageni 3 wakakaa nasi. Hivyo ndivyo ilivyoanza.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Brian yuko katika chumba hicho hicho, akiangalia fremu kadhaa ukutani. Yuko mbele ya fanicha nyembamba iliyo na taa, mmea na sanamu.

Brian
Watu wengi hawatambui Airbnb inamaanisha AirBed & Breakfast kwani awali tulipangisha vitanda vya hewa. Hii ndiyo risiti ya kwanza.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Brian ananyoosha kidole chake kwenye fremu iliyo na tiketi.

Mwendeshaji
Hili ni godoro la hewa?

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Anapozungumza, Brian anaonyesha ulaini wa godoro.

Brian
Hili ni godoro zuri sana na la starehe, kwa hiyo tumeboresha sana. Hili ni la kifahari zaidi kuliko godoro la hewa.

Hawa ni waanzilishi wenzangu 2, Joe na Nate. Hii ni mojawapo ya picha za mwanzo tukiwa pamoja.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Brian anashikilia fremu ya picha. Picha iliyomo ina vijana watatu wakiwa wanatabasamu. Nyuma yake, tunaweza kuona ramani kubwa ya dunia, nembo ya Airbnb iliyo kama sanamu na vitu vingine. Brian anaweka picha hiyo juu ya rafu.

Brian
Watu wanapoweka nyumba kwenye Airbnb waifanye ionekane na kinachofanya nyumba hii ionekane ni mimi ni mwanzilishi, ninaishi hapa, unaweza kupata historia kidogo kuhusu Airbnb ukiwa hapa.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Katika mfuatano wa haraka, tunaona klipu za mito miwili yenye umbo la herufi. Mmoja umeandikwa "Air" na mwingine "bnb"; picha kwenye fremu ya watu watatu wakiwa wanafanya kazi; masanduku ya chakula cha nafaka ya "Obama O'" na "Cap'n McCain's" na Brian kwenye chumba kilicho na ramani kubwa. Rafu tuliyoona hapo awali imethibitika kuwa dawati na unaweza kuona fanicha nyingine kwenye chumba hicho.

Mwongozaji
Mtu usiyemjua ataingia mtandaoni... awekee nafasi chumba hiki.

Brian
Ndiyo, ndiyo.

Mwongozaji
Kweli?

Brian
Kweli. Nilifanya hivyo miaka 15 iliyopita, nitafanya tena.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Picha inaonyesha sanduku na picha kwenye fremu ya mbao ya marafiki watatu wanaotabasamu. Karibu na sanduku, kuna sanamu ndogo za wanyama. Kisha, Brian anazungumza akiangalia moja kwa moja kwenye kamera akiwa na sura ya uhakika. Kisha, kamera inabadilika kutoka kwenye picha fupi ya uso wa Brian hadi picha pana inayoonyesha mikono na kiwiliwili chake.

Brian
Airbnb ilianzishwa wakati wa Poromoko la Uchumi. Mimi na mwenzangu Joe hatukuweza kumudu kulipa kodi. Hivyo tulikaribisha mgeni wa kwanza. Na huo ulikuwa mwanzo wa Airbnb.

Leo, kama wakati ule, watu wanatafuta njia za kujipatia pesa za ziada. Watu wengi zaidi sasa wanataka kukaribisha wageni. Lakini tunajua kuna vikwazo kadhaa kuweka eneo lako kwenye Airbnb. Moja, inaweza kuwa vigumu kuanza. Na pili, unaweza kuwa na wasiwasi kidogo kuhusu kuwa na wageni nyumbani kwako.

Tumekuwa tukishughulikia baadhi ya mawazo ili kutatua changamoto hizi. Leo, ninafurahi kukuonyesha kile ambacho tumeunda kwa ajili ya Toleo letu la Novemba 2022.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Kwenye mandharinyuma nyeupe, katika fonti nyeusi, imeandikwa, "Airbnb 2022 Winter Release."

Brian
Inaanza kwa Anza Kutumia Airbnb. Anza Kutumia Airbnb ndiyo njia mpya na rahisi sana ya kuiweka kwenye Airbnb, kuanzia kutangaza eneo lako hadi kuwekewa nafasi ya kwanza.

Anza Kutumia Airbnb imeundwa kutokana na wazo rahisi: njia bora ya kukusaidia kufanya kitu kipya ni kusaidiwa na mtu ambaye amekifanya hapo awali. Na tuna watu wengi kama hawa, Wenyeji wetu bora zaidi. Wanaitwa Wenyeji Bingwa na ni kiini cha Anza Kutumia Airbnb. Acha nikuonyeshe inavyofanya kazi.

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Brian anachukua simu yake na picha hiyo inapatanishwa na mandharinyuma nyeupe iliyo na simu mahiri mbele yake. Kwenye simu hiyo, programu ya Airbnb imefunguliwa ikiwa na dirisha ibukizi. Nusu ya juu ina mandharinyuma nyeusi na miduara yenye nyuso za Wenyeji Bingwa. Nusu ya chini ni nyeupe na imeandikwa, "Get one-to-one guidance from a Superhost." Kwenye sehemu ya chini, kuna baadhi ya herufi ndogo na chini yake, vitufe viwili. Cheusi kimeandikwa "Match with a Superhost" na cheupe kimeandikwa "Start on your own." 

Picha ya simu inavutwa karibu na tunaona sehemu ya chini, iliyoandikwa "Let's find you a Superhost," baadhi ya herufi ndogo chini yake na kitufe kinachosomeka "Next."

Brian
Bofya tu "Anza" na tutakukutanisha na Mwenyeji Bingwa wako, atakayekupa mwongozo wa moja kwa moja kwa kila hatua, bila malipo. Ili kukupa Mwenyeji Bingwa, tunakuuliza maswali mawili rahisi: eneo lako liko wapi na ni la aina gani?

Maelezo Kuhusu Maonyesho
Kwenye skrini ya simu, inasomeka: "Where's your place?". Chini ya maandishi haya kuna nafasi ya kuweka anwani na tena, kitufe cha "Next". Kisha skrini inabadilika na kuweka swali jipya: "Will guests have the place to themselves?" na machaguo mawili: "Yes, the place is all theirs" na "No, the place is shared." Chini yake, machaguo mawili yanaonekana: "Back" na "Get matched," ambayo yamejitokeza waziwazi.

Brian
Kisha Anza Kutumia Airbnb inatafuta kupitia maelfu ya Wenyeji Bingwa ili kupata anayekufaa karibu nawe.

Maelezo kuhusu maonyesho
Mandharinyuma inabadilika kuwa nyeusi na miduara kadhaa yenye nyuso inaonekana kuelea kote. Kisha, skrini ya simu inaangazia uso wa mwanamke wa makamo. Chini ya picha hiyo, kwa herufi nyeupe, imeandikwa: "Meet Jennifer," baadhi ya maelezo kumhusu, uzoefu wake kama mwenyeji na eneo lake. Hatimaye, chini ya skrini, kuna kitufe cha kuanza kupiga gumzo.

Brian
Kwa hivyo nimekutanishwa na Jennifer.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kamera inaangazia Brian akiwa kwenye simu ya video na Jennifer. Wanasalimiana na tunaweza kumwona Jennifer kwenye skrini ya simu iliyo mikononi mwa Brian.

Brian
Habari, Jennifer. Mimi ni Brian.

Jennifer
Habari Brian, nimefurahi kukutana nawe.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kamera inamwonyesha Brian akiongea, akiwa ameshikilia simu mkononi. Upande wake wa kushoto tunaona bakuli la matunda na nyuma yake kuna dirisha kubwa linaloingiza mwanga mwingi.

Brian
Anaweza kukusaidia kwa kile unachohitaji kutangaza eneo lako na kuwekewa nafasi ya kwanza. Unaweza kumwonyesha skrini yako, ili akusaidie kwa mambo kama kuchagua picha.

Maelezo kuhusu maonyesho
Uso wa Brian hufifia kwenye mandharinyuma nyeupe, ambapo skrini ya simu inaonekana na picha mjongeo inaonyesha fleti inayojikunjua kutoka sakafuni hadi darini.

Kwenye nusu ya chini ya skrini, imeandikwa "Step 1, Tell us about your place", ikifuatiwa na maandishi kwa herufi ndogo. Kisha, chini yake, vitufe viwili: "Back" na "Next," ambacho kinasisitizwa.

Uso wa Jennifer unaonekana kwenye dirisha dogo ibukizi, kamera inavuta picha karibu na tunaona picha kadhaa. Chini yake, imeandikwa "Choose at least 5 photos" na kuna kitufe cha "Upload".

Jennifer
Unataka kuhakikisha unapiga picha ya kila sehemu ambayo wageni wako watafikia katika nyumba yako.

Maelezo kuhusu maonyesho
Tunaona skrini nzima ya simu huku ikichagua baadhi ya picha zinazopatikana. Picha hizo zinalingana na picha ambazo tayari tumeziona kutoka kwenye nyumba ya Brian.

Brian
Andika kichwa.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kamera inavuta picha karibu na tunaona vitufe viwili kwenye sehemu ya juu: kimoja kimeandikwa "Save § exit" na kulia, kingine kimeandikwa "Questions?". Chini ya vitufe hivyo, kwa herufi kubwa, imeandikwa: "Now, let's give your house a title" na maelezo mafupi. Kisanduku cha maandishi kinaonekana tunapoona skrini nzima ya simu. Inawezekana kuweka hadi herufi 32.

Jennifer
Kifurahishe, kiwe cha kipekee, kitu ambacho ni maalumu au cha kipekee kwako.

Brian
"Zaidi ya airbed" kikoje?

Maelezo kuhusu maonyesho
Maneno "Beyond the airbed" yanaonekana kwenye sehemu ya kuandika.

Jennifer
Nakipenda.

Maelezo kuhusu maonyesho
Brian anapozungumza, yuko kwenye chumba angavu kilicho na matunda. Ameshikilia simu yake kwenye mkono mmoja na anaashiria kwa mkono mwingine. Brian anaonekana kuwa mkarimu na mwenye uhakika.

Brian
Baada ya kutangaza eneo lako, Mwenyeji Bingwa anaweza kukupa vidokezi vya kuliandaa, kuweka kalenda yako, hadi kumkaribisha mgeni wako wa kwanza. Yuko pamoja nawe kila wakati.

 Maelezo kuhusu maonyesho
Kwenye mandharinyuma nyeupe, huku programu ya Airbnb ikiwa imefunguliwa, skrini ya simu inaonyesha kichwa: "Choose who to welcome for your first reservation." Kisha, tuna machaguo mawili: "Any Airbnb guest" au "An experienced guest." Kamera inaangazia chaguo la pili. Kisha, picha inabadilika na tunaona Brian akizungumza na kamera.

Brian
Kwenye Anza Kutumia Airbnb, unaweza kuchagua kumkaribisha mgeni mzoefu kwa nafasi ya kwanza. Huyu ni mtu mwenye rekodi ya kuwa mgeni mzuri na mgeni mzuri anaweza kukusaidia kuwa na mwanzo mzuri.

Ndiyo hiyo. Nimetangaza chumba changu cha wageni kwenye Airbnb.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kwenye skrini ya simu, programu ya Airbnb ikiwa imefunguliwa, tunaona picha ya chumba cha wageni cha Brian ikiwa na kichwa alichochagua (Beyond the airbed). Chini yake, eneo la "San Francisco, California" na maelezo: "Private room, hosted by Brian." Kwenye sehemu ya chini, neno "aircover" chenye rangi bainifu za chapa na taarifa zaidi katika maandishi madogo. Kisha, matunzio ya picha yanaanza kuteleza na tunaona maelezo yote kuhusu chumba hicho cha kulala.

Brian

Tunajua kuna kikwazo kingine na hicho ni kuridhika kuwa na wageni nyumbani kwako. Na ndiyo sababu tuliunda AirCover.

Maelezo kuhusu maonyesho
Tunarudi kwa Brian, naye anawasilisha aircover. Kwenye mandharinyuma nyeupe, tunaona kwa herufi kubwa nyekundu "air" na nyeusi "cover." Chini yake, katika taipografia ndogo zaidi, "for Hosts."

Brian
Ni bila malipo, ulinzi kamili kwako na nyumba yako kila unapokaribisha wageni. Na leo, tunafanya maboresho makubwa kwenye AirCover kukupa ulinzi zaidi.

Maelezo kuhusu maonyesho
Brian anapozungumza, kamera inavuta picha karibu na uso wake na mbali zaidi, ikifunika kiwiliwili na mikono yake. Anaonyesha unyoofu, uaminifu na kuhisi hisia za wengine.

Brian
Moja ya maboresho yetu makubwa ni uthibitishaji wa utambulisho.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kwa maneno meusi, kwenye mandharinyuma nyeupe, imeandikwa "Identity verification."

Brian
Tangu mwanzo, tuligundua kwamba kumruhusu mtu aingie nyumbani kwako, lazima umwamini. Na ili kumwamini, lazima ujue ni nani. Vipi ikiwa tungeweza kuthibitisha kila mgeni anayeweka nafasi kwenye Airbnb? Hivyo ndivyo tutakavyofanya. Tunaanza leo kwa kuthibitisha wageni katika nchi 35. Hii inajumuisha 90% ya nafasi tulizowekewa. Majira ya kuchipua mwaka ujao, kila mgeni anayeweka nafasi kwenye Airbnb atathibitishwa.

Maelezo kuhusu maonyesho
Tena kwenye skrini ya programu, tunaweza kuona ukurasa kuhusu mgeni. Skrini hii inasomeka "About Priya" na kamera inaonyesha kwamba mgeni huyu ana utambulisho uliothibitishwa picha inapovutwa karibu. Hii inaonyeshwa kwa ikoni ya ngao nyeusi yenye alama nyeupe ya tiki ndani.

Brian
Mara tu mgeni atakapothibitishwa na akaweka nafasi, ni muhimu asiandae sherehe nyumbani kwako.

Maelezo kuhusu maonyesho
Anapozungumza, tunaweza kuona kwamba Brian anaashiria kwa mikono na kusisitiza maneno yake kwa ishara mbalimbali za uso.

Brian
Ndiyo maana tuliunda teknolojia ya kukagua nafasi iliyowekwa.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kwenye mandharinyuma nyeupe, kwa herufi nyeusi, imeandikwa "Reservation screening technology."

Brian
Teknolojia hii inaangalia mamia ya sababu kuzuia nafasi zilizowekwa zinazoweza kuwa na sherehe zisizoidhinishwa.

Maelezo kuhusu maonyesho
Kwenye skrini ya programu, tunaona ombi la kuweka nafasi, ambalo linaonekana kufunikwa na bango la rangi ya chungwa lenye ikoni ya ngao, inayoonyesha kwamba nafasi hii iliyowekwa imezuiwa. Tunasoma maandishi "This request was blocked" na maelezo ya kina katika maandishi madogo ya kijivu.

Brian
Tunazindua nchini Marekani na Kanada mwaka huu na ulimwenguni kote, majira yajayo ya kuchipua.

Maelezo kuhusu maonyesho
Tunaona $1,000,000 katika herufi nyeusi zilizojitokeza kwenye mandharinyuma nyeupe. Kisha, nambari zinasonga, zinaongezeka hadi $3,000,000.

Brian
Sasa, katika tukio nadra ambapo kitu kingetokea, tumeongeza ulinzi dhidi ya uharibifu ya AirCover kutoka USD milioni 1 hadi USD milioni 3 na sasa inajumuisha ulinzi kwa magari na boti zilizoegeshwa nyumbani kwako, pamoja na ulinzi kwa ajili ya sanaa na vitu vya thamani.

Maelezo kuhusu maonyesho
Miundo ya gari, boti na mchoro inaonekana kwenye skrini. Gari liko kwenye mduara wa kijivu. Meli iko kwenye mduara wa samawati hafifu unaofanana na maji na mchoro uko juu ya mduara unaofanana na sakafu ya mbao. Chini yake, kwa herufi, jina la kila kitu limeandikwa. "Cars," "Boats" na "Art § Valuables."

Brian
Hakuna kampuni yenye kitu kama AirCover.

Maelezo kuhusu maonyesho
Jedwali linalinganisha utendaji wa Airbnb na washindani wake. Kati ya alama 10 (alama 5 za kwanza ni za rangi ya kijivu hafifu), Airbnb ina alama 10 za tiki, wakati washindani wana alama 8 za mkasi ambazo ni nyekundu na alama 2 tu za tiki za kijani. Ulinganisho unatokana na taarifa za umma na matoleo ya bila malipo kutoka kwa washindani wakuu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2022.

Brian
Hilo ni Toleo letu la Novemba 2022. Anza Kutumia Airbnb hufanya iwe rahisi kuanza na kwa maboresho ya AirCover, tunakupa ulinzi zaidi.

Maelezo kuhusu maonyesho
Anapozungumza, tunaweza kumwona Brian akitabasamu, akiwa mwenye uhakika na urafiki.

Brian
Natumaini hii itarahisisha kuweka eneo lako kwenye Airbnb. Na ikiwa unakuja San Francisco na unahitaji sehemu ya kukaa, ningependa kukukaribisha.

Maelezo kuhusu maonyesho
Muziki unafifia